Trent kutua Real Madrid
Trent Alexander-Arnold yuko kwenye orodha ya beki wanaosakwa na Real Madrid, Newcastle wanamtaka Bryan Mbeumo, Arsenal wanajiandaa kumnunua Mohammed Kudus.
Real Madrid wanavutiwa sana na beki wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, wanapojiandaa kuimarisha safu yao ya ulinzi.
Newcastle United wamemjumuisha winga wa Cameroon Bryan Mbeumo kwenye orodha ya wachezaji wanaowataka, huku Brentford ikiweka bei ya pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Arsenal wanataka kumnunua winga wa West Ham wa Ghana Mohammed Kudus, 24, kama mbadala wa mshambuliaji wa Ubelgiji Leandro Trossard, 29, ambaye anawaniwa na klabu ya Al-Ittihad ya Saudia.
Mshambuliaji wa Reims kutoka Ivory Coast Oumar Diakite, 20, atakuwa kipaumbele cha Crystal Palace ikiwa mazungumzo ya kandarasi kati yao na mshambuliaji wao Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 27 yatagonga mwamba.
Manchester United na Chelsea wameungana na Tottenham katika mbio za kumsajili beki wa Denmark Patrick Dorgu, 20, kutoka Lecce.
Kiungo wa kati wa Uingereza Lewis O'Brien, 26, anatarajiwa kuhamia Los Angeles FC kwa dau la pauni milioni 7 wakati mkopo wake kutoka Nottingham Forest utakapokamilika Januari.
Kocha wa West Ham Julen Lopetegui anakabiliwa na shinikizo kubwa la kuondoka mapema baada ya kuufahamishwa na klabu kwamba matokeo lazima yaboreshwe.
Paris St-Germain na Randal Kolo Muani wako tayari kwa uhamisho wa mkopo wa mwezi Januari mwakani, wakiwa na chaguo la kununua, na baadhi ya vilabu vya Ligi ya Premia tayari vimewasilisha maombi ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 25.
Barcelona wanafuatilia hali ya Rafael Leao katika klabu ya AC Milan iwapo winga huyo wa Ureno, 25, atapatikana.